+255(0)232604380/1/3/4 | P.O. Box 9, Mzumbe, Morogoro - Tanzania

Aug 10, 2022 621times

MZUMBE WAJA NA MWAROBAINI WA NDOA ZA UTOTONI

Dkt. Seraphina Bakta, Mratibu wa Mradi wa Utafiti kuhusu changamoto za kiafya zitokanazo na Ndoa za Utotoni, akiwasilisha matokeo ya Utafiti wakati wa Warsha na wadau.  Dkt. Seraphina Bakta, Mratibu wa Mradi wa Utafiti kuhusu changamoto za kiafya zitokanazo na Ndoa za Utotoni, akiwasilisha matokeo ya Utafiti wakati wa Warsha na wadau.

Kaimu Makamu Mkuu wa Chuo, Prof. William Mwegoha, leo amezindua programu maalumu ya elimu na ufuatiliaji kimtandao “TOKOMEZA” pamoja na mwongozo wa mafunzo kwa Maafisa Ustawi wa Jamii, ambao utawasaidia katika kushughulikia changamoto ya ndoa za utotoni ambazo zimekuwa na madhara makubwa ya kiafya kwa watoto. 

Akizungumza wakati wa kumkaribisha Mgeni Rasmi, Mratibu wa Mradi huo ambaye pia ni Mtiva wa Kitivo cha Sheria cha Chuo Kikuu Mzumbe,  Dkt. Seraphina Bakta, amesema mradi huo ulianza mwaka 2020 na umehitimishwa mwaka huu kwa utafiti uliofanywa mkoani Dodoma na kuhusisha Wilaya mbili, na kwamba matokeo ya Utafiti huo yamepelekea kuanzishwa kwa Programu maalumu ya kimtandao ambayo wadau wataitumia kupata elimu ya sheria na kuripoti matukio mbalimbali ya ndoa za utotoni kwa wakati, ili hatua za haraka ziweze kuchukuliwa na Mamlaka husika. Amesema, mbali na programu hiyo, pia wameandaa mwongozo wa mafunzo ambao utatumiwa na Maafisa Ustawi wa Jamii na Maendeleo katika kutoa elimu  ya sheria kwa walengwa.

 Uzinduzi huo umefanyika Chuo Kikuu Mzumbe, Kampasi Kuu wakati wa kufunga warsha ya wadau ya uwasilishaji wa matokeo ya utafiti kuhusu Changamoto za ki-Afya zitokanazo na Ndoa za Utotoni nchini Tanzania, uliofanywa na Chuo Kikuu Mzumbe Kitivo cha Sheria kwa kushirikiana na Chuo Kikuu cha Antwerp Ubelgiji, kupitia mradi wa VLIR UOS.

Programu hiyo imelenga kuongeza uwelewa wa Maaafisa Ustawi wa Jamii kuhusu masuala ya sheria na miongozo iliyopo katika kushughulikia changamoto za ndoa za utotoni, pamoja na kufuatilia kwa karibu matukio ya ndoa za utotoni pindi yanapojitokeza, ili kuripotiwa na kushughulikiwa na Mamlaka zinazohusika kwa wakati. 

Ameahidi matokeo ya utafiti huo kuchapishwa katika majarida mbalimbali, pamoja kuanzisha mijadala ya kitaaluma na kisekta,  kwa kuhusisha wadau wote muhimu wa ndani, ili kuhakikisha matokeo ya Utafiti yanaleta matokeo chanya kwa jamii katika kukabiliana na changamoto ya madhara ya kiafya yatokanayo na ndoa za utotoni.

 Akihitimisha Warsha hiyo, Prof. Mwegoha amewashukuru wadau wa Maendeleo Serikali ya Ubelgiji, na wadau wengine wa ndani walioshiriki kufanikisha utafiti huo, ambao umelenga kutatua changamoto za ndoa za utotoni na madhara ya kiafya yatokanayo na ndoa hizo kwa watoto, ambazo kwa sehemu kubwa zinahusisha jamii ya watoto na familia masikini, wengi wao wakiishi vijijini. 

Ameahidi Chuo Kikuu Mzumbe, kuendelea kushirikiana kwa karibu na wadau wa mradi huo katika kuhakikisha matokeo ya utafiti huo yanakuwa na mwendelezo, na matokeo ya utafiti yanawafikia wadau wote muhimu, kama sehemu ya kuendelea kutafuta ufumbuzi wa kudumu wa tatizo la ndoa za utotoni ambazo zimekuwa zikikatisha ndoto wa watoto wengi katika jamii zetu.

“Chuo Kikuu Mzumbe kupitia mradi huu tunaahidi kuendelea kufuatilia kwa karibu na kutoa ushirikiano kwa wadau wetu wote wa ndani na nje, ili kuhakikisha tunakuwa sehemu ya kutatua changamoto za ndoa za utotoni na madhara yanayoambatana nayo” alisisitiza.

Akizungumza wakati wa kumkaribisha Mgeni Rasmi, Mratibu wa Mradi huo ambaye pia ni Mtiva wa Kitivo cha Sheria cha Chuo Kikuu Mzumbe,  Dkt. Seraphina Bakta, amesema mradi huo ulianza mwaka 2020 na umehitimishwa mwaka huu kwa utafiti uliofanywa mkoani Dodoma na kuhusisha Wilaya mbili, na kwamba matokeo ya Utafiti huo yamepelekea kuanzishwa kwa Programu maalumu ya kimtandao ambayo wadau wataitumia kupata elimu ya sheria na kuripoti matukio mbalimbali ya ndoa za utotoni kwa wakati, ili hatua za haraka ziweze kuchukuliwa na Mamlaka husika. Amesema, mbali na programu hiyo, pia wameandaa mwongozo wa mafunzo ambao utatumiwa na Maafisa Ustawi wa Jamii na Maendeleo katika kutoa elimu  ya sheria kwa walengwa.

Ameahidi matokeo ya utafiti huo kuchapishwa katika majarida mbalimbali, pamoja kuanzisha mijadala ya kitaaluma na kisekta,  kwa kuhusisha wadau wote muhimu wa ndani, ili kuhakikisha matokeo ya Utafiti yanaleta matokeo chanya kwa jamii katika kukabiliana na changamoto ya madhara ya kiafya yatokanayo na ndoa za utotoni.

Warsha hiyo imehudhuriwa na wadau mbalimbali zikiwemo Taasisi za Serikali, Mashirika yasiyo ya Kiserikali “NGO’s”, Maafisa Maendeleo ya Jamii, Wanasheria,  na wawakilishi  kutoka Chuo cha Antwerp Ubelgiji. 

****

Kaimu Makamu Mkuu wa Chuo, Prof. William Mwegoha, akizungumza na washiriki wa Warsha ya  uwasilishaji wa matokeo ya utafiti kuhusu Changamoto za ki-Afya zitokanazo na Ndoa za Utotoni nchini Tanzania, iliyofanyika Chuo Kikuu Mzumbe, Morogoro.

Prof. Wouter Vandenhole, Kaimu Mtiva wa Kitivo cha Sheria na Maendeleo ya Utafiti cha Antwerp nchini Ubelgiji, akichangia jambo wakati wa Warsha.

Kaimu Makamu Mkuu wa Chuo, Prof. William Mwegoha (Katikati), akizindua mwongozo wa mafunzo kwa wakufunzi wa madhara ya kiafya yatokanayo na ndoa za utotoni, wakati wa warsha ya wadau kujadili matokeo ya utafiti uliofanywa na Chuo Kikuu Mzumbe kwa kushirikiana na Chuo Kikuu cha Antwerp Ubelgiji. Kushoto ni Prof. Wouter Vandenhole, Kaimu Mtiva wa Kitivo cha Sheria na Maendeleo ya Utafiti, Antwerp Ubelgiji,  kulia ni  Dkt. Seraphina Bakta, Mratibu wa Mradi huo na Mtiva wa Kitivo cha Sheria cha Chuo Kikuu Mzumbe.

 Baadhi ya washiriki wa Warsha waKiwa katika picha ya pamoja. 

Go to top
JSN Educare is designed by JoomlaShine.com | powered by JSN Sun Framework